Zawadi ya Ushindi
Released: May 15, 1985
Publisher: East African Educational Publishers
Format: Paperback, 90 pages
to view more data
Description:
Idd Amini, kiongozi dhalimu kutoka nchi ya Uganda, alipoiteka sehemu ya nchi ya Tanzania na kuangamiza mamia ya watu wasiokuwa na hatia, serikali ya Tanzania iliamua kumkomesha kabla hajatekeleza maafa zaidi. Iliwatuma vijana wake wakapambane naye ili kusalimisha nchi yao.
Sikamona akiwa kijana barubaru aliukubali mwito wa serikali na kuingia vitani kukabiliana na Idd Amin na kikosi chake. Maisha ya Sikamona yalibadilika kabisa baada ya vita hivi. Hata ingawa walifaulu kumkomesha Idd Amin, Sikamona alibaki na makovu mengi yaliyoiharibu sura yake asijione kastahili kuitwa binadamu tena.
Ni yapi yatakayotokea watakapokutana na Rusia? Atapewa 'Zawadi ya Ushindi'?
We're an Amazon Associate. We earn from qualifying purchases at Amazon and all stores listed here.